Albamu ya Video

UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi. Vumilia L. Zikankuba, anapenda kuutaarifu Umma wa Watanzania kwamba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ataweka jiwe la msingi katika Mradi wa Ujenzi wa Vihenge na Maghala ya Kisasa. Sherehe hiyo itakayofanyika Makao Makuu ya NFRA yaliyopo Mtaa wa Kizota mjini Dodoma katika eneo la Viwanda siku ya Jumamosi tarehe 21 Aprili, 2018 saa 4.00 kamili asubuhi. WOTE MNAKARIBISHWA

Imewekwa: Apr 25, 2018