Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Kanda ya Makambako yamaliza zoezi la Ununuzi kwa mafanikio makubwa

Kaimu Meneja wa Wakala wa Taifa Kanda ya Makambako, Bwana Frank Felix amesema zoezi la ununuzi limekamilika kwa mafanikio makubwa na kwamba kila mwaka ubora wa mahindi umekuwa ni wa kuridhisha.

Bwana Frank Felix ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa mahojiano maalum na vyombo vya habari Ofisini kwake na kuongeza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Makambako imejivunia kutoa huduma ya kuwahakikishia soko la mahindi Wakulima wa Nyanda za Juu Kusini.

Kaimu Meneja ameongeza kuwa Kanda ya Makambako imekalisha zoezi hilo la ununuzi ambalo lilianza Mwezi Agosti na kukamilika tarehe 30 Septemba, 2017 na kuongeza kuwa Jumla ya tani 6,500.550 za mahindi zilinunuliwa kupitia Vukundi vya Wakulima na Vyama Vya Ushirika.

“Tumefanikiwa kununua kiasi hicho cha mahindi kupitia utaratibu huo wa Vikundi na Vyama vya Ushirika na kwa kweli, tumepata kiasi cha mahindi tani 6,500.550 ambapo mahindi yote yalikuwa ni mazuri.”Amekaririwa Bwana Frank Felix.

Bwana Frank ameendelea kusema Wakala Kanda ya Makambako imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuwaelimishaWakulima kuhusu ubora wa mahindi kupitia Maafisa Ubora wake kwa kusisitiza ubora kuanzia shambani kwenye uzalishaji, usafirishaji na uhifadhi na matunda yameanza kuonekana.

“Mwaka huu, tumenunua mahindi mazuri kutoka kwa Wakulima, jambo hili ni la kupongezwa na nitoe wito tu kwa Wakulima kuendelea na jambo hili”. Amekaririwa Kaimu Meneja.

Akieleza kuhusu majukumu ya Wakala wa Taifa wa Chakula Kanda ya Makambako, Bwana Frank amesema Wakala imekuwa ikitekeleza majukumu yake kupitia Kanda zake ikiwepo Kanda ya Makambako na kusema Mwaka wa Fedha uliopita yaani 2016/2017 Kanda ya Makambako ilisafirisha kiasi cha tani 5,000 za mahindi kwenda Kanda ya Kipawa ambayo inahudumia Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani.

“Kanda ya Makambako ipo kwenye eneo lenye uzalishaji mkubwa wa chakula yakiwemo mahindi na uwepo wa Kanda hii ni sehemu ya mkakati wa kutoa chakula kwenye eneo lenye uzalishaji mkubwa kwenye kwenye maeneo yenye upungufu”. Amekaririwa Kaimu Meneja, Kanda ya Makambako.

Kanda ya Makambako imekuwa ikihudumia Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Mkoa mpya wa Songwe ambapo inauwezo wa kuhifadhia kiasi cha nafaka tani 29,000 kati ya hizo tani 22,000 zinahifadhiwa katika maghala ya Makambako na tani 17,000 zinahifadhiwa katika Maghala ya Kituo cha Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved