Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo afungua mkutano wa kikazi kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula pamoja na timu ya Watendaji wa Wizara ya Kilimo ya Zanzibar

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (KILIMO) Mhandisi Mathew Mtigumwe leo amefungua mkutano wa kikazi wenye lengo la kubadirishana uzoefu na kujenga uwezo kati ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Mazingira.

Akimkaribisha, Katibu Mkuu, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula amesema kwa kipindi kirefu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imekuwa haina Wakala ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula kama ilivyokuwa NFRA Tanzania Bara na ndiyo maana ugeni huo umekuja Dodoma kwa ajili ya kujifunza.

Akifungua Mkutano huo, Mhandisi Mtigumwe amesema kuwa na akiba ya chakula ni jambo jema na kuongeza kuwa ni jukumu la Serikali kuhakikisha akiba ya chakula inakuwepo na kwamba upande wa Tanzania Bara, Serikali imekuwa ikitenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya kununua nafaka (Mahindi) kwa lengo kusaidia wananchi wakati wa uhitaji.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa ni nafasi nzuri kwa kila upande kujifunza kutoka kwa mwenzake hasa kwa kuzingatia kuwa asili ya watu wa kila upande wana aina ya chakula wanachokipenda na kuongeza kuwa Tanzania Bara mahindi ndiyo kipaumbele wakati Tanzania Visiwani mchele ndiyo kipaumbele.

Mkutano huo wa kikazi utakuwa wa siku moja na baadae ujumbe kutoka Zanzibar utapata nafasi ya kutembelea maghala ya Wakala wa Taifa Kanda ya Makambako.

 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved