Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Kikao cha kwanza cha Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kwa mwaka mpya wa fedha chafanyika Dodoma

Kikao cha kwanza cha kazi cha Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kimefanyika mkoani Dodoma kwenye Ofisi za Wakala wa Taifa Kanda ya Dodoma kwa lengo la kupanga na kuboresha mipango na utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa mwaka mpya wa fedha.

Kikao hicho cha kikazi ni cha kwanza kwa mwaka mpya fedha na kimeongozwa na Kaimu Mtendaji Mkuu, Bibi. Vumilia Zikankuba, Wajumbe wengine wa Kikao hicho ni Mameneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kutoka Kanda ya Kipawa, Makambako, Dodoma, Shinyanga, Arusha, Sumbawanga na Songea.

Wajumbe wengine ni Viongozi Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Mameneja kutoka Ofisi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (Makao Makuu, Dar es Salaam).

Akiongelea kuhusu kikao hicho cha kikazi, Kaimu Mtendaji Mkuu, Bibi. Zikankuba amesema moja kati ya mambo yaliyozungumziwa na kujadiriwa ni agenda ya ununuzi ya Wakala ambapo ununuzi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/2018 unataji kuanza Mwezi Julai. Mambo mengine ni kuboresha utendaji wa kazi za kila siku.

 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved