Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Kituo cha Mbozi kimekamilisha ujenzi wa Ghala Jipya

Kituo cha Mbozi kimekamilisha ujenzi wa Ghala Jipya

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Makambako kupitia Kituo cha Mbozi katika Mkoa wa Songwe hivi karibuni kimekamilisha ujenzi wa ghala jipya ambalo linauwezo wa kuhifadhi nafaka kiasi cha tani 5000.

Akizungumza na Wanahabari hivi karibuni Msimamizi wa Kituo hicho cha Mbozi, Bwana Elias Kangabwa amesema kuwa awali Kituo kilikuwa na uwezo wa kuhifadhi kiasi cha tani 12,000 za nafaka na ongezeko hilo la tani 5,000, sasa Kituo kitakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 17,000.

“Ongezeko hili ni hatua nzuri kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Kanda ya Makambako na maana yake ni kuwa Wakulima wengi wa Mkoa wa Songwe wanahakikishiwa soko la uhakika la kuuza mazao yao katika msimu ujao wa ununuzi kwani tutakuwa na nafasi kubwa ya kuhifadhi” Amekaririwa Bwana Elias.

Bwana Elias amesema ujenzi wa ghala hilo ulianza mwaka 2015 kwa kutumia fedha za ndani za Wakala na kuongeza kuwa, ujenzi umekwenda vizuri na kwamba hali ya ghala ni nzuri na limekamilika kwa zaidi ya asilimia 95 na kilichobaki ni kingo (Gutters) za kukusanyia maji yanayotoka kwenye paa kama mvua ikiwa inanyesha.

Akizungumzia kuhusu zoezi la ununuzi lililoisha hivi karibuni, Msimamizi huyo amesema kuwa kwa ujumla zoezi limekwenda vizuri na Kituo cha Mbozi kimefanikiwa kununua shehena ya mahindi yenye uzito wa tani 4,127.

Bwana Elias amesema zoezi la ununuzi lilianza rasmi tarehe 4/08/2017 na kukamilika tarehe 30/09/2017 na kuongeza kuwa kwa mwaka huu, Wakala wa Taifa Kanda ya Makambako Kituo cha Mbozi kilijikita katika kununua sehemu kubwa ya shehena ya mahindi kutoka kwa Vyama vya Ushurika na Vikundi vya Wakulima kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya.

“Napenda kuwashukuru Maafisa Ushirika na Wakuu wa Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Songwe kwa kufanikisha zoezi hili la ununuzi wa mahindi kupitia kwa Vikundi vya Wakulima na Vyama vya Ushirika” Amemalizia Msimamizi wa Kituo cha Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kituo cha Mbozi, Bwana Elias Kangabwa

 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved