Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Waziri wa Kilimo Afanya Ziara NFRA Kanda ya Arusha

Waziri wa kilimo MHE. Dk. Charles Tizeba amefanya ziara kwenye ofisi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya  Arusha ili kujionea Shughuli za Taasisi hii. Akiwa kwenye ofisi za Kanda ya Arusha Waziri alijionea Maghara ya Chakula na Chakula kilichohifadhiwa humo, pia alifanya kikao na Wafanyakazi wote wa Kanda hiyo.

Katika kikao hicho Waziri ameagiza NFRA kuwa sokoni wakati wote kwaajili ya kununua nafaka kila wanapouza nafaka zilizopo gharani na si kusubili mpaka msimu mpya unapoanza mwezi Julai pia ameagiza Wakala kuzingatia ubora wa nafaka katika ununuzi na uhifadhi na asingependa kusikia kuna nafaka zenye ubora hafifu kwenye hifadhi.

Waziri pia alipokea taarifa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala juu ya Mradi wa Upanuaji wa uwezo wa kuhifadhi nafaka na katika hilo Waziri aliagiza maandalizi yafanyike ya kuweka jiwe la msingi la Mradi. 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved