Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Kuhusu Sisi

 

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula – National Food Reserve Agency (NFRA) ni Taasisi ya Umma iliyo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika.  Wakala ulianzishwa chini ya sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997.

 Wakala ulinzishwa kwa madhumuni ya kuhakikisha usalama wa chakula nchini ili kukabiliana na upungufu wa chakula kwa njia ya kununua, kuhifadhi na kutoa chakula pale kinapohitajika kwa kuzingatia ufanisi na tija.

 

Dira:    

Dira ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ni kuwa taasisi yenye uwezo wa kukabiliana na upungufu wa chakula na kukisambaza kwa waathirika kwa wakati ifikapo mwaka 2020.

Dhamira:  

Dhamira ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ni Kuhakikisha usalama wa chakula nchini kwa kununua, kuhifadhi na kuzungusha akiba ya chakula kwa ufanisi na tija.  

 
 Majukumu mahususi ya NFRA ni pamoja na yafuatayo: 

(i) Kununua na kuhifadhi akiba ya chakula,

(ii) Kuzungusha (re-cycling) akiba ya chakula,

(iii) Kutoa chakula kwa waathirika waliokumbwa na upungufu wa chakula kwa maelekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa.

 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved