Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula

Matukio

29 May 2016

Maafisa ubora na watunza stoo watashiriki mafunzo ya kuwaweka tayari kwaajiri ya msimu unaokuja wa ununuzi wa chakula.

Kanda ya Arusha

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Arusha yanunua mahindi tani 4,500

Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Arusha Bwana Abilai Nyangasa wakati wa mahojiano maalum ofisini kwake hivi karibuni 


Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Arusha Bwana Abilai Nyangasa, amesema Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Arusha, imefanikiwa kununua kiasi cha shehena ya mahindi tani 4,500 wakati wa msimu wa ununuzi wa chakula wa 2016/2017.

Bwana Nyangasa amesema hayo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika Ofisini kwake hivi karibuni.

Bwana Nyangasa amesema Wakala imefanikiwa kununua kiasi hicho na kuongeza kuwa Wakala ilijikita katika kununua sehemu kubwa ya chakula kutoka kwa wakulima wadogo badala ya wafanyabiashara wakubwa kama ilivyokuwa awali.

Bwana Nyangasa amekaririwa akisema, “Ununuzi wa mahindi kwa mwaka huu kwa sehemu kubwa tuliuelekeza huko kwa kununua mahindi kutoka kwa wakulima wadogo”.

Bwana Nyangasa, ameongeza kuwa “katika msimu wa ununuzi wa 2016/2017 kulikuwana changamoto kadhaa, moja wapo ikiwa ni nchi jirani kukabiliwa na upungufu wa chakula, hali hiyo ilisababisha wageni wengi kuingia na kununua chakula kingi ambacho, hakijasindikwa na kuongeza kuwa ni nyema kama wafanyabiashara wa Tanzania, wakaiona fursa ya kununua chakula kutoka kwa wakulima na kukisindika ili wageni kutoka nchi jirani waje kununua unga badala ya mahindi.

“Ni nyema wafanyabiashara wakawa wanaona mbali na kuisaidia Serikali ambayo imekuwa ikiweka mazingira bora ya biashara kwa ajili ya watu wote na si maana kwamba tusifanye biashara na majirani zetu, hapana ila biashara ifanyike lakini tunaposema tunaenda kwenye uchumi wa viwanda ni pamoja na kutengeneza ajira kwa watu wetu kwa kusindika mazao badala ya kuyauza yakiwa hayajasindikwa.

Bwana Nyangasa, ametoa mfano zao la mahindi na kuongeza kuwa unaposindika unga wa mahindi, kwanza una muakikishia Mtanzania ajira, pili unakuwa na uhakika wa chakula cha mifugo kinachotokana na pumba pamoja na mambo mengine lakini shughuli nzima ya usindikaji, hutumia umeme na vifungashio (maguni) ambavyo vyote, vinatengenezwa hapa nchini wa Watanzania.

Akizungumzia kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa maghala ya kisasa (Silos) katika Kanda ya Arusha, Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Kanda ya Arusha, Bwana Nyangasa, amesema eneo la ujenzi lilimeshapatikana na kwamba upanuzi huo utafanyika katika Mji wa Babati na Ofisi ya Wakala ipo kwenye hatua za mwisho za kupata hati ya kumiliki viwanja 10 eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 34,933.7.

 

Copyright © National Food Reserve Agency 2014. All Rights Reserved